Friday, January 27, 2012

MACHOZI NA DAMU

Machozi na Damu

Intro:
      Hii Ni real life
      (Come on, come on )*2
         
Verse one
Natoa hisia halisi,
Za life tunayopitia,
Usiku na mchana zinaenda zikijirudia,
Hatuoni mabadiliko ambayo tunakuzudia,
Wakati mwingine tuzidiwa hadi tunawaza kujiua,
Ila pendo la Mola hutuwezesha kushikilia,
Hebu vuta picha ya umaskini na dhiki tunazopitia,
Ni vigumu kwendelea unapokosa anayekuzimia,
Hawaoni bidii yetu ni shida zetu wanafurahia,
Nanajenga taswira ya raha kwenye nchi mpya,
Napaona akilini ila wahuni washatangulia,
Ndugu yangu namzimia ila hakuna tunakoelekea,
Shetani ashamteka sasa ana nia ya kuniua,
Masela wenye nyoyo safi hushindwa kujizuia,
Kwa mazishi tunapoomboleza ni hisia huumia,
Hakuna ajuaye siri ya peponi tunakoelelea,
Life is so crazy naomba nguvu za kuniokoa,
Niione asubuhi njema nitokwe machozi ya kufurahia,
Usidanganyike na tabasamu hizi ni za bandia,
Natamani maisha ya utotoni ju ni ya kufurahia,
Sasa unless tushirikiane hatutabadilisha hii dunia.
         (Ah come on).

                   Chorus*2

        Hivi ndivyo tunavyoishi,
        Duniani ki ujambazi,
        Tunaendelea kusurvive,
        Kwa machozi na damu

 Verse two

Nadondokwa na machozi,
Napoitazama dunia,
Mapenzi yameginda sumu hatuna cha kufurahia,
Mipango ya kando inazidi kuvunja familia,
Najiuliza kama ni yangu ni nini nitajifanyia?
Jibu linanikosa nachutama naanza kulia,
Ingawa hayajanipata nahisi uchungu wanayopitia,
Inauma sana kuona mtu ambaye unamzimia,
Akimpenda mwingine bila yeye kukufikiria,
Sio ajabu kupandwa mori hata wivu ukakuua,
Disappointments en desperation zimetufanya kukimbilia,
To the old women’s arms tukidhani kwao tutatulia,
Fahamu wanaumiza ujana na zaidi ninapotoza njia,
Ngono inakata kiu tu sio kukufanya kufurahia,
Naombea madem wadogo ju ni vigumu kuwakatia,
Hawana mapenzi ya dhati ni mikwanja wanaangalia,
Wakisha pajikwa mimba ndio anaanza kutufikiria,
Wakiwa na watoto bila baba na magonjwa ya kuua,
As if hatuwadeserve kabla vibabu kuwapitia,
Hata Yule dem msupa wanaume wananga’ang’ania,
Kuna mwenye anamwepa kwa vile ashamtia.
     (Ah hala)


          Hivi ndivyo tunavyoishi,
         Duniani ki ujambazi,
        Tunaendelea kusurvive,
       Kwa machozi na damu.

Verse three
Napofumbua macho ni dhiki ninajionea,
Unyanyasaji na mauaji hali sio ya kufurahia,
Sasa hatutaki kuona mama ya mtu akilia,
Kuwa mtoto wake amepiwa kaaga dunia
Ila tukitaka haki zetu itatubidi hata kuua,
Kwa kelele cha mdomo hakuna atakayetusikia,
Kuna vita mitaani na pembe zote za dunia,
Badala ya vita vya umasikini ni vita vya kuua,
Tunagonganishwa na mabwenyenye ambao wamendelea,
Wanajifanya wanachukiana ila ni sahani moja wanakulia,
Hali zingine hazitabadilika itatubidi kuitikia,
Hii ni life ya kubaatisha ya hakika tuaingojea,
Majambazi wa bungeni na polisi ndio wanaotuua,
Badala ya kulipa ushuru ni mishahara wanajiongezea,
Heli kuwa maiti kama hatuna sababu ya kufurahia,
Mamangu na babangu heshima kubwa nawapatia,
Hamkuzaa fala na ni kwa shida mlinilea,
Nawe Naomi Nyaboke na kuappreciate na nakuzimia,
Naomba Mungu asiwasahau katika nchi mpya,
Tujumuike na Malaika mbinguni tukifurahia.
    (Ah nimechoka).

     
          Hivi ndivyo tunavyoishi,
         Duniani ki ujambazi,
        Tunaendelea kusurvive,
        Kwa machozi na damu.





Outro:
              Unless we change ourselves,
             We can’t change the world,
            Let’s change the way we treat each other,
           Deepac Braxx
          (The Heavyweight Messiah).

No comments:

Post a Comment